KPA wabebwa ubingwa wa FIBA Rwanda
6 Novemba 2023Imewabwaga Rwanda Energy Group (REG) timu ya nishati ya Rwanda kwa vikapu 87-53 jumamosi mjini Kigali.
Timu ya mpira wa kikapu Kenya Ports Authority KPA imemaliza mechi zote bila kufungwa, katika mchezo wa fainali imeifunga Club ya nishati Energy Group, kwa vikapu 87-53 jumamosi.
Soma pia: Rayon Sport yashindwa kutamba katika ligi kuu Rwanda
Timu ya Kenya Ports Authority wanawake, imetawazwa mabingwa wa Ukanda wa V katika shindano la mpira wa kikapu maarufu'' FIBA Africa Women Basketball League'' kufuatia ushindi wa vikapu 87-53 dhidi ya REG Rwanda Energy Group Timu ya nishati ya Rwanda.
Kocha wa KPA Antony Ojukwu Oloo alisema ‘'Naweza kusema kuwa shindano lilikuwa gumu na limekuwa zuri ka sababu tulikuwa tumejitayarisha vya kutosha, nashukuru pia na ninapongeza wachezaji wangu na uongozi kwa jumla. Niseme pia kwamba ulinzi (defense yangu) imenisaidia sana kupata ushindi''
Kocha wa REG mshindi wa pili Mukaneza Esperance, "Katika mchezo wa fainali tulianza na nguvu nyingi pamoja na kwamba kulikuwepo tofauti, imeonekana wapinzani walikuwa juu yetu, tulipambana hadi dakika ya mwisho. Tulikuwa na mchezaji wetu hatari kwa jina Nyota Mireille ambaye hakucheza alipata jeraha."
Timu hizo mbili moja kwa moja zimefuzu kushiriki fainali ya kombe la Afrika FIBA Africa Women Basketball League' itakayofanyika nchini Misri tarehe 8-17, 2023.
Equit Bank ya Kenya wamemaliza kwenye nafasi ya tatu kufuatia ushindi wao dhidi ya timu ya Uganda ya JK Lady.
Mshindano hayo yaliyokuwa yakifanyika Kigali kuanzia tarehe 28 Octoba hadi 04 Novemba 2023 yametamatika mwishoni mwa juma.
Tuangazie upande wa soka, Torsten Frank Spittler mjerumani mwenye umri wa miaka 61 ametangazwa na Shirikisho la soka nchini Rwanda FERWAFA kuwa kocha mpya wa Timu ya taifa ya soka ya Rwanda Amavubi akichukua mikoba ya mhispania Carlos Alos Ferrer.
Spittler hana historia nzito ya ukufunzi. Hapo kabla alikuwa mkurugenzi wa ufundi katika shirikisho la soka nchini Msumbiji na Siera Leonne.
Aliwahi pia kuwa mkufunzi msaidizi wa timu ya taifa ya Ujerumani kwa wachezaji walio chini ya miaka 16.
Rwanda ina kabarua kuchuana na Zimbabwe tarehe 15 Novemba 2023 kabla ya kuipokea Afrika ya kusini tarehe 21 mwezi huu mjini Huye kusini mwa Rwanda kusaka tikiti ya kombe la dunia mwaka 2026.
//Christopher Karenzi (DW Kigali)