KUALA LUMPAR : Malaysia yatangaza hali ya hatari
11 Agosti 2005Matangazo
Serikali ya Malaysia imetangaza hali ya hatari nchini humo kufuatia kiwango cha juu cha uchafuzi wa hewa katika pwani ya magharibi ya nchi hiyo, ukiwemo mji mkuu Kuala Lumpur. Shule zote zimefungwa na wakaazi wametakiwa wabakie ndani ya nyumba zao.
Maofisa wanasema moshi mwingi uliotanda katika anga umesababishwa na visa yapata 1,000 vya moto uliowashwa kusafisha vichaka katika kisiwa cha Sumatra nchini Indonesia, ili ardhi iweze kutumiwa kwa kupanda mimea.