KUALA LUMPUR: Malaysia ipo tayari kuchangia vikosi Lebanon
4 Septemba 2006Matangazo
Waziri mkuu wa Malaysia Abdullah Ahmad Badawi amesema,nchi yake ipo tayari kupeleka vikosi vya kulinda amani nchini Lebanon lakini ingali ikingojea ruhusa kutoka Umoja wa Mataifa.Malaysia imejitolea kupeleka wanajeshi 1,000 nchini Lebanon kuimarisha vikosi vya Umoja wa Mataifa,ingawa Israel imepinga kwa sababu nchi hizo mbili hazina uhusiano wa kibalozi.Malaysia imeuhimiza Umoja wa Mataifa kuwaruhusu wanajeshi wa Malaysia kujiunga na vikosi vya kimataifa UNIFIL licha ya Israel kupinga kuruhusu nchi ambazo hazikulitambua taifa la Kiyahudi.