1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kuala Lumpur:Mamia waandamana Malaysia.

28 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG35

Mamia ya waandamanaji wanaopinga vita pamoja na wanaharakati za kisiasa wamejaribu kuvamia eneo la mkutano wa mazungumzo ya usalama katika bara la Asia katika mji mkuu wa Malaysia, Kuala Lumpur, wakidai wafanye mazungumzo na waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice.

Waandamanaji hao walivunja vizuwizi, na kuwalazimisha polisi kushikana ili kutengeneza uzio utakaowazuwia waandanaji hao kuingia katika ukumbi wa kituo cha mikutano cha mjini Kuala Lumpur ambako mawaziri wengine 25 wa eneo hilo walikuwa wakikutana.

Maandamano hayo yaliongozwa na mkwe wa kiume wa waziri mkuu Abdullah Ahmad Badawi.

Polisi waliopanda farasi walipambana na makundi ya waandamanaji wakipeperusha bendera na mabango ambayo yameandikwa izuieni Israel. Iokoe Lebanon.

Kiasi mtu mmoja amejeruhiwa katika msukumano huo.