1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaLebanon

UN: Lebanon inakabiliwa mgogoro mbaya kabisa

6 Oktoba 2023

Lebanon inakabiliwa na moja ya mgogoro mbaya zaidi duniani, ambapo takriban watu milioni 4 wanahitaji msaada wa kibinadamu ikiwa ni pamoja na chakula.

https://p.dw.com/p/4XBu2
Mmoja ya jamaa wa wahanga wa mlipuko mkubwa katika bandari mjini Beirut, Agosti 4, 2022, ambao pamoja na mengineyo ulizidi kudhoofisha uchumi wa taifa hilo lililokabiliwa pia na mzozo wa muda mrefu wa kisiasa
Mmoja ya jamaa wa wahanga wa mlipuko mkubwa katika bandari mjini Beirut, Agosti 4, 2022, ambao pamoja na mengineyo ulizidi kudhoofisha uchumi wa taifa hilo lililokabiliwa pia na mzozo wa muda mrefu wa kisiasaPicha: Houssam Shbaro/AA/picture alliance

Taarifa hiyo ni kulingana na Imran Riza ambaye ni afisa wa Umoja wa Mataifa.

Riza amesema nusu ya watu hao hawatapata misaada kutokana na ukosefu wa ufadhili.

Tangu 2019, Lebanon imekuwa ikikabiliwa na mfululizo wa majanga. Wanasiasa wa nchi hiyo ambao wanalaumiwa kwa miongo kadhaa ya ufisadi na usimamizi mbovu wa mali ya umma, wamekuwa wakipinga mageuzi ya kiuchumi na kifedha yaliyopendekezwa na jumuiya ya kimataifa.

Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya kibinadamu amebainisha kuwa Lebanon imekuwa bila rais kwa karibu mwaka mmoja na taasisi zake nyingi hazifanyi kazi. Watu wanaohitaji msaada ni raia wa Lebanon, wahamiaji pamoja na wakimbizi kutoka Syria na Palestina.