Kumbukumbu ya miaka mitano ya janga la Tsunami Japan
11 Machi 2016Ilipotimia saa nane na dakika 46, majira ya Japan,watu waliohudhuria kumbukumbu hiyo waliinamisha vichwa vyao pamoja na wakaazi wa maeneo yaliyoathiriwa kutoa heshima na kukumbuka wenzao waliokufa mnamo saa sawa na hiyo tarehe kumi na moja mwezi Machi mwaka 2011, pale tetemeko la Tsunami lenye ukubwa wa 9.0 lilitokea katika bahari Pasific
Maji mengi yalibomoa majengo na kusomba vitu na kuathiri vinu vya nyuklia vya Fukushima Daiichi hali iliyosababisha kuvuja kwa mionzi hatari ya nyuklia kuwahi kushuhudiwa tangu mwaka 1986. Kwenye hotuba yake mfalme Akihoto alihuzunishwa na wale waliolazimishwa kuhama makwao kutokana na ajali hiyo.
"Nahisi Uchungu moyoni nikikumbuka watu ambao bado hawawezi kurejea makwao kwa kuwa maeneo mengine hayawezi kushi watu tena," alisema mfalme Akihito
Hali katika eneo la Fukushima ambapo viwanda vya nyuklia viliathirika ingali ya tahadhari. Hali hiyo ilisababisha maelfu ya watu wanaokadiriwa kufikia laki moja kuhama na kuacha nyumba pamoja na mali yao.
Serikali ya Japan inasema itachukua miongo minne kuondolewa kwa mabaki ya viwanda vya nyuklia vilivyoharibiwa na mengine yakaingia baharini kutachukua zaidi ya miongo minne.
Mnamo Jumanne mahakama ya Japan iliamuru kampuni ya nishati Kansai kusitisha kwa muda viwanda vyake vipya vya nishati kwa misingi ya usalama, hali inayo
Hata hivyo waziri mkuu Shinzo Abe amekariri haja ya Japan kuzalisha nishati kwa njia ya nyuklia akisema mikakati ya kuunda upya viwanda zaidi itaharakishwa
''Taifa letu lisilo na utajiri wa raslimali haliwezi kufanikiwa bila nishati ya nyuklia ambayo inaleta utengamano wa nishati, na kwa kuzingatia mahitaji ya kiuchumi na suala la mabadiliko ya tabia-nchi,'' alisema Waziri Mkuu Shinzo Abe
Ahadi ya serikali ya Japan imefanya Wajapani kuwa na shaka, kuhusu usalama wa nishati ya nyuklia.
Mwandishi: John Juma
Mhariri: Gakuba Daniel