1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kundi la ADF lafanya shambulizi Uganda

Josephat Charo
13 Oktoba 2023

Naibu msemaji wa jeshi la Uganda UPDF Deo Akiiki amesema wapiganaji watano wa ADF walilivamia lori lililokuwa limebeba vitunguu.

https://p.dw.com/p/4XVpG
Jeshi la Uganda lilipelekwa Kongo kuwasaka waasi wa ADF
Jeshi la Uganda lilipelekwa Kongo kuwasaka waasi wa ADFPicha: Alain Uaykani/Xinhua/picture alliance

Kundi la waasi la Allied Democratic Forces ADF linaloendesha shughuli zake nchini Congo lenye mafungamano na kundi linalojiita dola la kiislamu limemuua angalau mwanamume mmoja na kumjeruhi mwingine wakati lilipolishambulia lori magharibi wa Uganda usiku wa kuamkia leo katika shambulizi linaloelezwa kuwa la nadra.

 Naibu msemaji wa jeshi la Uganda UPDF Deo Akiiki amesema wapiganaji watano wa ADF walilivamia lori lililokuwa limebeba vitunguu katika kona ya barabara ya Katojo, kijiji kinachopatikana kiasi kilometa tatu kutoka mpaka wa Congo.

Katika taarifa yake Akiiki amesema mmoja kati ya watu wanne waliokuwa ndani ya gari hilo, alipigwa risasi na kuuliwa, mwengine hajulikani aliko, na wa tatu alijeruhiwa vibaya na mwanamke mmoja kutoroka bila majeraha.

Akiiki pia amesema vikosi vya jeshi la Uganda vinawafuatilia washambuliaji.