1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kundi la G20 kusaidia soko la ajira lisiporomoke

24 Aprili 2020

Mawaziri wanaohusika na masilahi ya wafanyakazi na ajira wa kundi la mataifa yaliyostawi kiuchumi, G20, wameahidi kulisaidia soko la ajira lisiporomoke huku janga la virusi vya corona likiathiri ajira kote ulimwenguni.

https://p.dw.com/p/3bM9j
Saudi Arabien | G20-Finanzministertreffen in Riad
Picha: Getty Images/AFP/F. Nureldine

Mawaziri wa kundi hilo ambalo kwa sasa linaongozwa na Saudi Arabia wamesema kwamba mataifa yao yataendelea kutafuta njia za kusaidia biashara na waajiri, hasa biashara ndogo ndogo, na za kati, kuweza kutunza ajira na kusaidia wafanyakazi walioathirika katika kipindi hiki kigumu.

Shirika la Kazi Duniani ILO lilionya Jumanne kuwa athari za kiuchumi za mripuko wa virusi vya corona zinawaumiza vibaya wafanyakazi na waajiri katika sekta zote.

Lakini shirika hilo la Umoja wa Mataifa limesema kwamba wakati wowote vikwazo vikiondolewa, basi wafanyakazi wanapaswa kurudi kazini wakiwa na ulinzi sahihi, ili kuzuia kutokea tena kwa janga hilo.

Chanzo: afpe