Wapiganaji wa kundi la waasi wa M23 wanaopambana na jeshi la Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameondoka kwenye mji mdogo wa Kibumba ambao wamekuwa wakiushikilia kwa zaidi ya mwezi mmoja. Je, kuondoka kwao kutakuwa na athari gani katika mzozo unaoendelea mashariki mwa DRC? Sikiliza mahojiano kati ya Amina Abubakar na mchambuzi wa masuala ya kanda ya Maziwa Makuu, Ali Mali.