1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kwaheri msimu wa 2015/16 wa Bundesliga

16 Mei 2016

Bayern Munich ilinyakua taji lake la nne mfululizo ikiwa ni rekodi mpya, wakati Borussia Dortmund wakimaliza wa pili. Hata hivyo upande wa mkia wa ligi ndio ulishangaza.

https://p.dw.com/p/1Iogn
Deutschland Fußball Bundesliga 2016 34. Spieltag Bayern München - Hannover 96 Meisterschale
Picha: picture-alliance/dpa/A. Gebert

Bayern ilimwambia kwaheri Pep Guardiola baada ya miaka mitatu licha ya kuwa hakuweza kunyakua Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya lakini kushinda Bundesliga kwa mara ya nne mfululizo ni kitu ambacho wachezaji wa Bayern wamejivunia kama anavyoeleza nahodha Philipp Lahm "Tulitaka kuvunja rekodi, yani kuwa mabingwa wa Ujerumani kwa mara ya nne mfululizo. Na tumefanya hilo. Lilikuwa lengo kubwa kwetu. Na ahsante kwenu nyote, kwa sababu mlitushangilia sana sio tu katika mechi za Bundesliga lakini pia katika za Champions League.

Baada ya kupata mafanikio katika ligi ya Uhispania, na Ujerumani, sasa Pep anaelekea England ambapo ana hamu ya kuonja kandanda la Uingereza katika klabu ya Manchester City. Karl-Heinz Rummenigge, mwenyekiti wa Bayern amemshuruku Mhispania hiyo kwa kazi yake nzuri na mabingwa hao. "Ningependa kukushukuru sana mpendwa Pep. Uliponiambia mwezi desemba kuwa umeamua kufanya kitu kipya, pia ulisema: ninataka kuondoka Bayern nikiwa rafiki, na sasa katika mwezi huu wa Mei, nnaweza kusema kuwa utaondoka Bayern ukiwa rafiki. Sio kwa sababu tumekuwa mabingwa, sio kwa sababu tunalenga kunyakua taji la pili wiki ijayo, lakini kwa sababu miaka mitatu nawe hapa ilikuwa na umuhimu mkubwa

Pengo baina ya nafasi mbili za kwanza na timu nyingine kwenye ligi lilikuwa pointi kubwa – pointi 18 baina ya nambari mbili na tatu, na 36 kati ya nambari moja na tano, ambayo ndiyo nafasi ya kwanza ya kucheza katika Europa League

Fußball 1. Bundesliga Christian Gentner und Daniel Ginczek vom VfB Stuttgart
Stuttgart wametumbukia katika ligi ya divisheni ya piliPicha: picture alliance/Pressefoto

Katika nafasi za kandanda la Ulaya hakukuwa na mabadiliko yoyote, Bayer Leverkusen ilikuwa ya tatu wakati Borussia Moenchengladbach ikimaliza ya nne.

Vilabu vya majina makubwa ndivyo vilivyoumia, baada ya Hanover na VfB Stuttgart, mabingwa wa Bundesliga 2007, kushushwa daraja. Mabingwa wa 2004 Werder Bremen waliponea chupuchupu, wakati Eintracht Frankfurt watacheza dhidi ya timu ya daraja ya pili Nuremberg katika mchuano wa mchujo kuamua kama watabaki au kushuka daraja. Mabingwa wa divisheni ya pili SC Freiburg wamepandishwa ngazi pamoja na RB Leipzig.

Mshambuliaji wa Bayern Robert Lewandowski, aliibuka mfungaji bora kwa kupata magoli 30 goals, mbele ya mwenzake wa Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang, aliyetikisa wavu mara 25.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri:Yusuf Saumu