LAGOS: Balozi ndogo zimefungwa nchini Nigeria
18 Juni 2005Matangazo
Marekani,Uingereza na Ujerumani zimefunga ofisi zake za ubalozi mdogo katika mji wa Lagos nchini Nigeria.Mashirika ya habari yamemnukulu mwana diplomasia mmoja aliesema kuwa habari za upelelezi kuhusu wanamgambo wa kigeni wa kiislamu zimeonyesha kuwa kuna vitisho,hasa dhidi ya Marekani nchini Nigeria.Balozi ndogo za Uingereza na Ujerumani zimefungwa kwa sababu ya wasi wasi wa Marekani kuhusu usalama.Inasemekana kuwa kiongozi wa mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda,Osama Bin Laden ameitaja Nigeria kama ni nchi ya „kukombolewa“.