1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LAGOS: Human right watsch yashutumu wakuu wa Nigeria kutesa na kuuwa wapinzani-

2 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFvz
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu Human Right Watsch, limeshtumu wakuu wa Nigeria, kwamba wamekua wakitesa na kuuwa wapinzani.

Shirika hilo linasema watu ambao walipinga ziara ya Rais George W Bush nchini Nigeria, iliyofanyika mwezi julai uliopita walikamatwa wakateswa.

Walifanyiwa hivo hivo pia wapinzani, wakati wa kampeni za uchaguzi wa Rais uliofanyika mwezi Aprili, na wengi wao walouwawa.

Kwa mujibu wa shirika hilo la kutetea haki za binaadamu Human Right Watsch, vitendo hivyo vya wakuu wa Nigeria vimekua vikiendelea hadi wakati huu.

Human Right Watsch linazitolea mwito nchi wanachama wa Jumuia ya madola Common Wealth, kujadili swali la ukiukaji wa haki za binaadamu nchini Nigeria, katika mkutano wa Jumuia hiyo utakaofanyika katika mji mkuu wa Nigeria Abuja, kuanzia tarehe tano hadi tarehe nane mwezi huu.