LAGOS: Kifo cha kwanza kimethibitishwa Nigeria kuhusika na H5N1
1 Februari 2007Matangazo
Maafisa wa afya nchini Nigeria wamethibitisha kifo cha kwanza cha binadamu kilichosababishwa na homa ya mafua ya ndege katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.Wanigeria 4 wanashukiwa kuwa wamefariki kutokana na virusi vya H5N1,lakini uchunguzi uliofanywa haukuweza kuhakikisha kuhusu wahanga wengine 3.Kifo kilichothibitishwa ni cha mwanamke kutoka mji mkuu wa biashara,Lagos ambae mama yake pia ni miongoni mwa kesi zingine tatu ambazo hazikuweza kuthibitishwa.Ugonjwa huo ambao husababisha kifo,uligunduliwa Nigeria kwa mara ya kwanza,Februari mwaka jana.