LAGOS: Machafuko mapya yazuka Nigeria
11 Julai 2006Matangazo
Si chini ya watu 8 wameuawa na wengi wengine wamejeruhiwa katika mapambano yaliyozuka upya kati ya vikosi vya usalama na makundi ya waasi katika mji wa Onitsha,kusini-mashariki mwa Nigeria.Mapambano hayo yalizuka baada ya vikosi vya polisi kujaribu kuyafukuza makundi hayo kutoka mji huo.