LAGOS: Marekani na Uingereza zafunga ofisi zake za ubalozi NIgeria
17 Juni 2005Matangazo
Marekani imefunga ubalozi wake mjini Abuja na ubalozi wake mdogo mjini Lagos kufuatia kile ilichokiita ukosefu wa usalama. Lakini kwa mujibu
wa msemaji wa Ubalozi huo hana taarifa zozote kuhusiana na tukio lolote la kiusalama.
Polisi wa Nigeria wanachunguza madai hayo.
Kufuatia hatua hiyo ya Marekani Uingereza pia imefunga Ubalozi wake mjini Lagos kufuatia wasiwasi huo.
Duru za kidiplomasia nchini humo zimesema kwamba Marekani imepokea vitisho kutoka kwa wapiganaji wa kigeni walioko nchini Nigeria.
Hata hivyo wanadiplomasia na wachunguzi wanasema hakuna ushahidi wowote hadi sasa wa kuonyesha kundi linaloongozwa na Osama Bin Laden la Alqaeda lipo nchini humo.