LAGOS: Mfanyakazi wa kigeni wa kampuni ya mafuta auawa kusini mwa Nigeria
23 Novemba 2006Matangazo
Mtu mmoja miongoni mwa waliotekwa nyara ameuawa na mwingine amejeruhiwa wakati polisi wa usalama wakijaribu kuwaokoa mateka 7 wafanyakazi wa kigeni wa kampuni ya mafuta ambao walitekwa nyara na watu wenye kuwa na silaha kusini mwa Nigeria. Kampuni ya mafuta ya Italy, Eni, imesema katika taarifa kwenye mtandao wake kwenye Internet, kwamba wafanyakazi wake 6 wamenusurika katika mapigano ambayo yametokea katika operesheni ya uokozi ya majeshi ya Nigeria. Hata hivyo, taarifa hiyo ya kampuni ya mafuta ya Eni, haikutaja uraia wa wafanyakazi hao.