1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LAGOS: Nigeria yaomboleza

24 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEOs

Nigeria imetangaza siku tatu za kuomboleza vifo vya watu wote 117 waliafariki dunia katika ajali ya ndege iliyotokea nchini humo. Ndege hiyo aina ya Boeng 737 ya shirika la ndege la Bellair, ilikuwa njiani ikieleka mjini Abuja wakati ilipoanguka katika kijiji cha Lissa, magharibi mwa mji wa Lagos mda mfupi baada ya kuondoka mjini Lagos.

Rais Olusegun Obasanjo anaongoza uchunguzi wa kutathmini kilichoisababisha ajali hiyo na ameamuru bendera zipeperushwe nusu mlingoti kama ishara ya heshma kwa walliouwawa katka ajali hiyo. Wafanyikazi wa dharura wanaendelea na kibarua kigumu cha kuziondoa maiti za abiria kutoka kwa mabaki ya ndege hiyo yaliyotapakaa kwenye eneo la ajali. Polisi wamepata vifaa vya kunasia sauti na wanatumai kupata mwelekeo mzuri katika uchunguzi wao.

Maofisa wa ngazi ya juu wa Nigeria na jumuiya ya uchumi ya mataifa ya Afrika Magharibi, ECOWAS ni miongoni mwa wahanga waliokufa katika ajali hiyo. Mtayarishi wa vipindi vya televisheni kuhusu uchumi wa Afrika Kusini, Adele Lorenzo, ni miongoni mwa waliofariki dunia katika ajali hiyo.

Rais wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki, amemtumia risala za rambirambi rais Obasanjo, kufuatia kifo cha mkewe, Stella, na ajali hiyo ya ndege.