LAGOS: Wafanyakazi wa kigeni watekwa nyara Nigeria
3 Juni 2007Matangazo
Nchini Nigeria,watu waliobeba bunduki wamewateka nyara wafanyakazi 6 wa kigeni wa kampuni la RUSAL,katika mji wa Ikot Abasi ulio kusini mashariki ya nchi.Kwa mujibu wa duru za usalama, wafanyakazi hao walikamatwa baada ya fleti yao kuripuliwa kwa miripuko.Afisa mmoja amesema, Warusi 3 na wananchi 2 wa Afrika ya Kusini ni miongoni mwa hao waliotekwa nyara na vile vile dreva wao,raia wa Nigeria aliuawa katika shambulizi lililofanywa saa za alfajiri