LAGOS:Rais Nigeria atengua kandaras ya mamilioni ya dolai iliyotolewa na Obasanjo
7 Agosti 2007Matangazo
Rais Umaru Yar Adua ametoa amri ya kusitishwa kwa kandarasi yenye thamani ya mamillioni ya dola iliyotolewa kwa kampuni moja na utawala wa Rais wa zamani Olesegun Obasanjo.
Kandarasi hiyo yenye thamani ya dola millioni 145 ilikuwa ni ya ujenzi wa vituo vya afya kote nchini Nigeria na ilipewa kampuni inayoaminika kuwa ni ya aliyekuwa msaidizi wa Obasanjo.
Rais Umaru amesema kuwa kandarasi hiyo ilitolewa kinyume na sheria za utoaji kandarasi.
Mwezi uliyopita Rais huyo alisitisha uuzwaji uliyokuwa na utata wa viwanda viwili vya kusafisha mafuta kwa kundi la wafanyabiashara wanaoaminika kuwa na uswahiba na rais huyo wa zamani.
Nigeria inachukuliwa kuwa moja ya nchi zenye kiwango cha juu cha rushwa.