1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LAGOS:Tume ya Uchaguzi ya Nigeria yaongeza muda wa usajili

31 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCWV

Tume ya Uchaguzi nchini Nigeria inaongeza muda wa wapiga kura kujisali kwa siku tatu katika matayarisho ya uchaguzi wa rais na wabunge unaopangwa kufanyika mwezi Aprili.Shughuli hiyo ya usajili iliyoanza mwezi Oktoba mwaka jana imeshaongezwa muda mara moja kwa majuma machache sasa inakamilika siku ya Ijumaa.Hayo ni kwa mujibu wa msemaji wa Tume hiyo ya Uchaguzi Andy Ezeani.

Uongozi nchini Nigeria ulitoa siku za mapumziko kwa wafanyikazi wa serikali ili kuwawezesha raia kusajiliwa.

Miezi ya kwanza miwili ya shughuli hiyo ya usajili ilizongwa na matatizo ya kiufundi na mipango kwani baadhi ya wapiga kura hawakufahamu wakati shughuli hiyo ilipoanza vilevile mashine za usajili.

Uchaguzi huo wa Aprili unatazamiwa kuwa wa kwanza kutokea baada ya uongozi wa kidemokrasia ikikumbukwa kuwa nchi y Nigeria imekabiliwa na mapinduzi ya kijeshi hapo awali.