LAGOS.Wajenzi wasiopungua 10 wakwama baada ya jengo kuporomoka Nigeria
26 Mei 2005Matangazo
Wajenzi wasiopungua kumi wamekwama katika jengo lililoporomoka katika mji wa kusini mwa Nigeria ulio na mafuta wa Port Harcourt.
Jengo hilo lililoanguka siku ya jummane limewauwa watu ambao idadi yao haijajulikana.
Polisi wamesema Mazingira magumu katika sehemu hiyo yamezuia shughuli za kuwaokoa manusura kutoka kwenye vifusi vya jengo hilo.
Taarifa ambazo hazijathibitishwa zinasema watu wasiopungua 40 walikuwa ndani na nje ya jengo hilo wakati lilipoporomoka.