1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LAGOS:Wanamgambo wa Nigeria watishia kuhujumu visima vya mafuta.

21 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEYx

Vikundi vya wanamgambo wanaotaka kujitenga nchini Nigeria,vimetishia kuviripua visima vya mafuta pamoja na mabomba yanayosafirisha mafuta,baada ya kueleza kuwa kiongozi wao ametiwa mbaroni kwa kushukiwa kuingiza silaha na kutishia usalama wa taifa.

Kwa mujibu wa naibu kiongozi wa kikundi cha wanamgambo kilichopigwa marufuku cha Niger Delta People’s Volunteer Force,Alali Horsefall,wanamgambo wake wapo tayari kutekeleza hujuma hizo na ameipa idara ya polisi ya Nigeria hadi mchana huu kumuachia huru kiongozi wao.

Wanamgambo hao walifanya maandamano usiku kucha katika mitaa ya mji wa kusini wa Port Harcourt unaotoa mafuta,wakidai kuachiwa kwa kiongozi wao Alhaji Dokubo Asari,ambaye walisema anashikiliwa na polisi na hivi sasa amesafirishwa hadi katika mji mkuu Abuja.

Wakaazi wa mji huo wamedai kusikia milio ya risasi usiku kucha.

Hata hivyo polisi wa Nigeria hadi sasa wamekataa kukiri au kukanusha kama wanamshikilia Asari.