Lavrov aikosowa "sera ya hatari" ya Marekani
19 Oktoba 2023Matangazo
Lavrov aliyasema hayo alipowasili na kufanya mazungumzo na maafisa wa Pyongyang siku ya Alkhamis (Oktoba 19), akiongeza kuwa ana wasiwasi wa kuongezeka kwa shughuli za kijeshi za Marekani na washirika wake katika ukanda huo.
"Tunapinga hatua hiyo isiyojenga na iliyo ya hatari." Alisema Lavrov.
Soma zaidi: Jumuiya ya ASEAN yahofia mizozo mipya
Aidha mwanadiplomasia huyo mkuu wa Urusi alisema nchi yake inaunga mkono "mchakato wa mazungumzo ya mara kwa mara kuhusu masuala ya usalama, katika Rasi ya Korea".
Lavrov alisema Moscow, Beijing na Pyongyang zinataka kupendekeza "njia mbadala" ili kupunguza mivutano katika eneo hilo.
Mikutano ya Lavrov mjini Pyongyang inatarajiwa kuweka msingi wa ziara ya baadaye ya kiongozi wa Urusi, Vladimir Putin.