1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Lavrov aitembelea Korea Kaskazini

Josephat Charo
18 Oktoba 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Segei Lavrov amewasili nchini Korea Kaskazini, huku wasiwasi wa nchi za Magharibi ukiongozeka kuhusu kuimarika kwa mahusiano kati ya nchi hizo mbili washirika wa kihistoria.

https://p.dw.com/p/4XhRy
Russland Moskau | Russischer Außenminister | Sergei Lavrov
Picha: Sergei Ilnitsky/REUTERS

Msemaji wa Ikulu ya Kremlin aliliambia shirika la habari la Urusi, TASS, kwamba ziara ya siku mbili ya Lavrov inaweka msingi wa maandalizi ya ziara ya Rais Vladimir Putin wa Urusi itakayofanyika siku za usoni.

Soma zaidi: Marekani, Korea Kusini, Japan kufanya mazoezi ya kijeshi

Lavrov aliwasili Pyongyang akitokea Beijing, ambako Putin alimpongeza Rais Xi Jinping wa China akimumuita rafiki yake wa miaka mingi wakati alipohudhuria mkutano kuhusu mradi mkubwa wa China wa ujenzi wa miundombinu na barabara.