Lawama kali dhidi ya WTO:
18 Januari 2004WTO yalaumiwa vikali katika mkutano wa Bombay:
BOMBAY. Hii leo katika Mkutano wa Kimataifa wa Maswali ya Kijamii mjini Bombay, India, wapinzani wa siasa mpya ya kiliberali ya mfumo wa utanda wazi, wamelilamu vikali Shirika la Kimataifa la Biashara, WTO. Kiongozi wa Wakulima wa Kifaransa José Bové alisema kote duniani wakulima ndiyo wahanga wa kwanza wa siasa ya WTO. Asili miya 60 ya watu wanaokumbwa na balaa na njaa duniani ni wakulima. Mlinzi wa Mazingira kutoka India, Bibi Vandah Shiva alilaumu vikali mapatano ya kuhifadhiwa haki za mbegu. Mapatano hayo ya WTO yanatia moyo wizi wa kuibiwa ujuzi wa watu masikini katika nchi zinazoendelea, alisema. Kwa mfano makampuni ya nchi za viwanda yanataka kuhifadhi haki ya kuzalisha mchele wa Basmati kutoka Himalaya na aina za ngazo kutoka India. Hapo jana aliyekuwa Kamishna wa UM wa Haki za Binadamu, Bibi Mary Robinson alitoa mwito wa kufikiwa mapatano ya kuzuiya uenezaji wa silaha ndogo. Alisema kuwa silaha ndogo kama bastola ndizo silaha za kuangamiza za enzi zetu. Kila mwaka wanauawa raiya wapatao 500,000 kupitia silaha hizo. Hasa hasa katika Kolumbia, Sierra Leone na Chechenia silaha hizo hutumiwa kukiuka haki za binadamu, alisema. Akasisitiza mwito wake kuwa hadi mwaka 2006 lazima ufikiwe Mkataba wa Kimataifa wa Ukaguzi wa Silaha Ndogo.