1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Le Pen apandishwa kwa chuki dhidi wa wageni

24 Aprili 2012

Duru ya mwanzo ya uchaguzi wa Ufaransa imeibua wasiwasi kwa kura nyingi alizopata mgombea uraisi mwenye siasa kali za mrengo wa kulia, Marine Le Pen, ambaye anatumia chuki dhidi ya wageni kama bango lake kuu la kisiasa.

https://p.dw.com/p/14kB9
Marine Le Pen
Marine Le PenPicha: Reuters

Licha ya mgombea uraisi wa chama cha kijamaa, Francois Hollande, na mtetezi wa kiti cha hicho kutoka chama cha kihafidhina, Nicolas Sarkozy, kuingia duru ya pii ya uchaguzi hapo tarehe 6 Mei, macho hasa yanaelekezwa kwa Le Pen, ambaye wafuasi wake wanaongezeka kwa kasi.

Katika makala hii ya Mwangaza wa Ulaya, Oummilkheir Hamidou anamulika jinsi wapiga kura wa kambi ya mwanasiasa huyo inayoeneza chuki dhidi ya wageni watakavyoweza kushawishi matokeo ya uchaguzi duru ya pili.

Kusikiliza makala hii, tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Makala: Mwangaza wa Umoja wa Ulaya
Mtayarishaji/Msimulizi: Oummilkheir Hamidou
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman