1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lebanon yapata ahadi ya misaada ya zaidi ya dola bilioni 10

6 Aprili 2018

Waziri wa fedha wa Lebanon Ali Hassan Khalil  amesema serikali yake inaihamasisha jamii ya kimataifa kuiunga mkono Lebanon katika mipango ya uwekezaji ili kuimarisha uchumi wa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/2vcyH
Frankreich Paris Libanon Konferenz
Picha: Reuters/P. Wojazer

Ahadi hizo zimejumuisha kiasi cha dola bilioni 4 katika mkopo wa Benki ya Dunia, zingine dola bilioni 1.35 zikiwa ni mkopo kutoka Benki ya Ulaya kwa ajili ya Ujenzi na Maendeleo. Maafisa wa Lebanon wamesema Saudi Arabia pia imethibitisha ahadi yake iliyotoa awali ya kuipa Lebanon mkopo wa dola bilioni 1. Lebanon imekumbwa na misukosuko ya vita vya nchi jirani ya Syria kwa muda wa miaka saba ambapo Lebanon ndio mwenyeji zaidi ya wakimbizi milioni 1 kutoka Syria.

Nchi hiyo inatafuta misaada ya fedha kwa ajili ya marekebisho ya miundombinu yake na pia kuinua uchumi wa nchi hiyo. Waziri Mkuu Saad al-Hariri amefahamisha kwamba uchumi wa Lebanon umeshuka hadi kufikia chini ya asilimia 1 kutoka kiwango cha wastani wa asilimia 8.

Waziri mkuu wa Lebanon Saad al Hariri
Waziri mkuu wa Lebanon Saad al HaririPicha: picture-alliance/ MAXPPP/ Z. Kamil

Waziri mkuu wa Lebanon Saad al Hariri amesema Lebanon inahitaji washirika ili kufikia malengo yake. Amesema ''Lebanon haiwezi kufanikiwa peke yake, inahitaji msaada wa jumuiya ya kimataifa kwa njia ya michango na mikopo ya dhamana, ambayo italeta tumaini ili matarajio ya serikali yaweze kutekelezwa. Ninawaomba mzingatie maendeleo mazuri ya hivi karibuni, ambayo ni sababu tosha ya kuimarisha utulivu wa Lebanon. Ninaamini hii sio kwa utulivu wa Lebanon tu bali ni utulivu wa kanda nzima na dunia yote. "

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian und Adel al-Dschubair
Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Jean-Yves Le DrianPicha: Getty Images/AFP/F. Nureldine

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian amesema Lebanon kama mfano mzuri wa siasa za pande nyingi, ustahimilivu na uwazi katika Mashariki ya Kati iliyogawanywa na vita. Uchaguzi wa bunge utakaofanyika katika muda wa mwezi mmoja ujao unatoa muda muafaka wa kuonyesha kuwa nchi hiyo inaungwa mkono.

Mkutano juu ya Lebanon wa mjini Paris Ufaransa
Mkutano juu ya Lebanon wa mjini Paris UfaransaPicha: Reuters/E. Feferberg

Mkutano huo ni mfululizo wa mikutano mitatu, wa kwanza ulifaniyka huko mjini Roma, Italia mwezi wa pili ambako ahadi za zaidi ya dola milioni 550 zilitolewa kwa ajili ya kulisaidia jeshi la Lebanon na mkutano wa tatu umepangiwa kufanyika huko mjini Brussels, Ubelgiji baadae mwezi huu. Mkutano huo utazingatia kuisidia Lebanon katika juhudi zake za kuwakirimu wakimbizi wa Syria.

Kushoto: Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron. Kulia: Waziri mkuu wa Lebanon Saad al Hariri
Kushoto: Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron. Kulia: Waziri mkuu wa Lebanon Saad al HaririPicha: picture-alliance/MAXPPP/A. R. Ammar

Ufaransa, ambayo ilikuwa na mamlaka juu ya Lebanon katika nusu ya kwanza ya karne ya 20, imekuwa inaongoza juhudi za kuiimarisha nchi hiyo. Wakati Hariri alipotangaza kujiuzulu kwake mnamo mwezi Novemba mwaka uliopita, katika hatua ya kushangaza ambapo wengi waliona kwamba mwanan mfalme wa Saudi Arabia Mohammed Bin Salman alihusika, Rais Emmanuel Macron aliingilia kati kwa kumkaribisha Saad al Hariri kwenda Paris kwa ajili ya mazungumzo ambapo baadaye alirudi nchini mwake Lebanon.

Mwandishi:Zainab Aziz/RTRE/AFPE/DPAE

Mhariri:Josephat Charo