1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Leo ni siku ya kimataifa ya wanawake duniani

8 Machi 2023

Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake, miji mikuu kote ulimwenguni itashuhudia maandamano na mikutano ya hadhara, ukiwemo Madrid.

https://p.dw.com/p/4OOBR
Spanien Protest gegen das Regime im Iran | Barcelona
Picha: Paco Freire/SOPA/ZUMA Press Wire/picture alliance

Wanawake wanapanga kufanya maandamano makubwa kote ulimwenguni leo kutetea haki ambazo zinazidi kushambuliwa. Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake, miji mikuu kote ulimwenguni itashuhudia maandamano na mikutano ya hadhara, ukiwemo Madrid, ambako mitaa ya katikati ya mji huo hujaa rangi ya samawati, inayohusishwa na haki za wanawake. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gutteres alionya mapema wiki hii kuwa haki za wanawake zinatoweka mbele ya macho zetu, akisema suala la usawa wa jinsia litachukua karne nyingine tatu ili kutimizwa.

Katika mkesha wa Siku ya Kimataifa ya Wanawake, Umoja wa Ulaya uliweka vikwazo dhidi ya watu binafsi na vyombo vinavyoonekana kuhusika na unyanyasaji na ukiukaji wa haki dhidi ya wanawake.