Lewandowski ataka kikosi cha Bayern kiimarishwe
5 Agosti 2019Mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski anataka klabu yake kusajili wchezaji bora ambao wataweza kuleta athari ya haraka kikosini badala ya wachezaji wenye uwezo tu.
Akizungumza baada ya kipigo cha mabo 2-0 dhidi ya mahisimu wao wakubwa Borussia Dortmund katika kombe la Ujerumani la Super Cup siku ya Jumamosi, Lewandowski alilalamikia ukosefu wa wachezaji wanaoweza kubadili mchezo miongoni mwa wachezaji wa akiba wa Bayern na alionekana kuhoji sera ya uhamisho ya klabu.
"bila shaka wachezaji chipukizi katika benchi wana uwezo , hii ni kweli, lakini wakati mwingine unahitaji mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa moja kwa moja ambaye anaweza kuingia uwanjani na kuisaidia timu," Lewandowski alisema.
Ikilinganishwa na Dortmund , ambayo imekiimarisha kikosi chake kwa kiasi kikubwa majira haya ya kiangazi, Bayern imepata saini ya walinzi wa kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa Benjamin Pavard na Lucas Hernandez , wakati Arjen Robben, Frank Ribery , James Rodriguez, Mats Hummels na rafinha wameondoka katika klabu hiyo. Mshambuliaji Mjerumani Fiete Arp amewasili akitokea Hamburg SV licha ya kuwa haifahamiki iwapo atabakia na klabu hiyo ama atapelekwa kwa mkopo kwa msimu mmoja katika klabu nyingine.