1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lewandowski kujiunga na Bayern msimu ujao

10 Januari 2014

Usajili wa mapema wa mchezaji nyota wa Borussia Dortmund Robert Lewandowski ambaye atajiunga na Bayern Munich mwanzoni mwa msimu ujao unaendelea kuzusha maswali miongoni wma mashabiki

https://p.dw.com/p/1AohH
Robert Lewandowski Fußballspieler ARCHIV 2012
Picha: picture-alliance/dpa

Wengi bila shaka wamejiuliza ni vipi mshambuliaji huyo ataweza kuihudumia klabu yake kwa dhati wakati akifahamu kuwa tayari atajiunga na mahasimu wa Dortmund msimu ujao.

Lewandowski hata hivyo ameahidi kuwa atajitoa mhanga na kuichezea BVB katika kipindi kilichosalia cha msimu kabla ya kugura. Mshambuliaji huyo wa Poland amesema ataisaidia Dortmund kutimiza malengo yake katika kipindi kilichosalia cha msimu ijapokuwa anafahamu kuwa baadhi ya mashabiki hawakubaliani na uamuzi wake wa kuihama Dortmund.

Kocha wa Dortmund Jurgen Klopp ameutaja uamuzi wa Lewandowski kuhama klabu hiyo na kujiunga na mabingwa wa Bundesliga kuwa ni “usio tatizo lolote” kwa sababu klabu hiyo ilifahamu muda mrefu kuwa mchezaji huyo alitaka kuondoka punde mkataba wake utakapokamilika mwishoni mwa msimu huu.

Kwingineko, kiungo mshambuliaji wa Ujerumani Sydney Sam atajiunga na Schalke kutoka mahasimu wao wa Bundesliga Bayer Leverkusen kuanzia msimu ujao. Schlake imesema Sam atapewa mkataba wa miaka minne hadi 2018. Inaaminika ada ya uhamisho ni euro milioni 2.5. Sam mwenye umri wa miaka 25 alijiunga na Leverkusen mwaka wa 2010, na ameifungia magoli saba msimu huu, pamoja na kuichezea timu ya taifa ya Ujerumani mara tano katika mwkaa wa 2013.

Fußball Bundesliga 7. Spieltag Hannover 96 Bayer Leverkusen
Schalke wameinyakua saini ya mchezaji kiungo wa Bayer Lervekusen Sydney SamPicha: imago/Kolvenbach

Leverkusen wako katika nafasi ya saba katika Bundesliga, huku Schalke wakiwa nyuma yao katika nafasi ya saba, ijapokuwa timu zote mbili zimefika kazika awamu ya kumi nha sita za mwisho katika Champions League, ambako Leverkusen itapambana na Paris St Germain na Schalke itashuka dimbani na Real Madrid.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman