1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Liberia baada ya Uchaguzi

12 Oktoba 2011

Shughuli ya kuhesabu kura bado inaendelea nchini Liberia baada ya zoezi la uchaguzi mkuu uliofanyika jana.

https://p.dw.com/p/12qYa
Raia wa Liberia walipiga kura jana tarehe 11.10.2011Picha: DW

Uchaguzi huu ni wa pili kufanyika tangu nchi hiyo kuingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe miaka 14 iliopita.

Baadhi ya matokeo ya kura yanaonyesha kivumbi kikali kati ya Rais anayemaliza wadhifa wake na mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel Ellen Johnson Serleaf na mwanasiasa wa upande wa upinzani na aliyekuwa mwanadiplomasia wa umoja wa mataifa Winston Tubman.

Winston Tubman Liberia Präsidentschaftskandidat
Winston Tubman mwanasiasa wa Upinzani LiberiaPicha: picture alliance/dpa

Tayari wachambuzi wa mambo ya kisiasa nchini humo wanasema iwapo mambo yatajkwenda salama katika uchaguzi huu na matokeo kutolewa bila ya udanganyifu wowote basi nchi ya Liberia itapata tena nafasi ya kufufua uwekezaji katika sekta zake za kawi ili kuinua uchumi wa taifa hilo maskini barani afrika.

Tume ya uchaguzi nchini humo NEC katika taarifa yake iliotolewa hapo jana usiku imesema matokeo ya mikoa itakuwa tayari kutolewa ifikapo siku ya alhamisi. Hata hivyo kulingana na katiba ya nchi hiyo mda wa siku kumi na tano unapaswa kuchukuliwa katika kuhesabu na kutoa matokea ya uchaguzi mkuu.

Uchaguzi huo uliofanyika hapo jana uliripotiwa kuendeshwa kwa amani huku waangalizi wa kimataifa wa kura wakisema hawakupokea ripoti ya visa vyovyote vya ghasia katika nchi hiyo ilio na idadi ya watu millioni 4.

Afisa mmoja wa mambo ya kisiasa na utoaji misaada ya kibinaadam wa umoja wa Afrika nchini Liberia Prosper Addo amesema kulingana na uchaguzi huo kufanyika kwa mani sasa naona liberia ikisongea karibu katika kupatikana kwa demokrasia.

Hali ya kuzuka kwa ghasia za baada ya uchaguzi zilionekaniwa wakati wa utata wa matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2005 wakati rais Ellen Johnson Serleaf akichukua utawala kama rais wa kwanza mwanamke barani afrika.

Mwakilishi wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ellen Margreth amesema majeshi ya kulinda amani ya umoja huo yako nchini Liberia kudumisha amani tangu kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe. Margreth amewasihi wa liberia kudumisha amani na kukubali matokeo ya uchaguzi.

Mwandishi. Amina Abubakar RTRE

Mhariri Othman Miraji