Liberia yafanya uchaguzi wa rais na bunge
10 Oktoba 2023Amani ndilo suala muhimu miongoni mwa wapiga kura mnamo wakati uchaguzi ukiendelea, katika nchi hiyo ambayo bado ina makovu ya vita mfululizo vya wenyewe kwa wenyewe.
Alipochaguliwa mwaka 2017 Rais Weah aliahidi kutengeneza nafasi za ajira na kuwekeza katika elimu, lakini wakosoaji wanasema ameshindwa kutimiza ahadi zake.
Weah ana nafasi kubwa ya kushind uchaguzi huo dhidi ya wagombea 19 wanaowania urais lakini huenda akakabiliwa na uchaguzi wa duru ya pili mapema mwezi Novemba ikiwa hakuna mgombea atakayepata wingi wa kura unaohitajika katika duru ya kwanza.
Mamia ya watu walijitokeza mapema Jumanne kupiga kura katika mji mkuu Monrovia.
Vyama vikuu vya upinzani vimeahidi kwamba uchaguzi wa rais na bunge utafanyika kwa amani. Uchaguzi huo ni wa kwanza kufanyika tangu Umoja wa Mataifa ulipokamilisha tume yake ya amani Liberia mnamo 2018.