1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Liberia yakabiliwa na migogoro ya ardhi

21 Februari 2018

Liberia inakabiliwa na migogoro ya ardhi kati ya wananchi na wawekezaji wa kigeni ikiwa ni wiki sita tangu kuapishwa kwa Rais Geoge Weah.

https://p.dw.com/p/2t4e7
Äthiopien Addis Abeba Afrikanische Union Gipfel Guterres George Weah
Rais George Weah wa Liberia (katikati)Picha: Reuters/T. Negeri

Liberia inakabiliwa na migogoro ya ardhi kati ya wananchi na wawekezaji wa kigeni ikiwa ni wiki sita tangu kuapishwa kwa Rais Geoge Weah ambaye kabla ya kushika madaraka aliapa kupambana na tatizo hilo ambalo limedumu kwa muda mrefu sasa.

Kidir, Mzee katika kijiji cha Gbah kilicho kwenye Kaunti ya Bomi yupo mstari wa mbele katika mgogoro wa kitaifa wa ardhi, ulioanza katikati mwa karne ya 19 na hapo ndipo anapoingia Rais George Weah, aliyeapishwa wiki sita zilizopita ambaye baada ya kuapishwa aliliambia taifa kwamba wananchi wanahitaji kuelezwa kwa uwazi juu ya mambo muhimu kama vile ardhi, uhuru wa kujieleza, mgawanyo wa rasilimali za taifa na majukumu.

Anakumbuka Mwezi Oktoba mwaka uliopita, wakati wafanyakazi kutoka Muungano wa vyama vya ushirika vya wafanyakazi kutoka Malaysia, Sime Darby walipowasili kwenye eneo hilo na kuanza kulifanyia kazi  likiwa ndilo pekee lenye uwazi katika msitu uliojaa michikichi.

Aliwahi kuandika barua kwa moja ya viwanda vinne vikubwa vya kutengeneza mafuta ya mawese ikiomba kiwanda hicho kuondoka kwenye ardhi yao ili waweze kupata maendeleo.

Kidir amesema licha ya makubaliano ya kuacha nafasi kati ya mashamba na makaazi kwenye vijiji kama Gbah michikichi  huota hadi mlangoni  lakini yeye kama watu wengine wana shauku ya kufahamu ni nini serikali na viwanda wamekubaliana.

Foto Pulitzer Preis 2015 Ebola AUSSCHNITT
Moja ya eneo inapolimwa michikichiPicha: picture-alliance/dpa/Daniel Berehulak/The New York Times

Makubaliano hayatambuliwi na wananchi

Wakazi wa vijijini wanasema hawafahamu kuhusu makubaliano yaliyofikiwa baina ya serikali na makampuni ya kimataifa wanapoingia mikataba ya muda mrefu na hawana rasilimali za kutosha wachimbaji wanapojitokeza nyuma ya nyumba zao.

"Karibu makubaliano yote yaliyofikiwa hayajahitimishwa kwa kupewa idhini , licha ya juhudi zinazofanywa na makampuni", ameeleza naibu mkurugenzi wa shirika la kutetea haki na rasilimali Africa, Lien De Brouckere.

Kwa mujibu wa ripoti ya maendeleo ya umoja wa mataifa Liberia, iliyo magharibi mwa Afrika moja ya nchi zenye umasikini uliokithiri inashikilia nafasi ya 177 kati ya 187. Pamoja na uwepo wa madini ya chuma, zao la mpira na mafuta ya mawese bado nchi hiyo inabaki kuwa mfano mbaya  kwa wawekezaji wa kigeni na vyanzo vya mapato.

Ali kaba, kutoka taasisi ya maendeleo endelevu nchini humo alisema siku zote migogoro ya ardhi imekuwa ni tatizo lakini hivi sasa watu wana uelewa zaidi kutokana ha harakati za taasisi za kimataifa.

Serikali ya nchi hiyo inatarajiwa kurejea upya muswada wa zamani wa haki za ardhi ambao wanaoutetea wanasema ulidhoofishwa na bunge la wawakilishi  mwaka 2017 kabla ya kuzuiwa na seneti.

Kabla ya serikali ya sasa, Mtangulizi wa Weah, utawala wa Ellen Sirleaf Johnson aliyekuwa madarakani kwa miaka kumi na miwili makubaliano ya miongo kadhaa yalipitiwa upya ama kubadilishwa kwa lengo la kuchunguza mikataba ya ardhi.

Liberia, ilianzishwa na watumwa walioachiwa huru kutoka marekani mwaka 1847 na kuanzisha mfumo rasmi wa umiliki ardhi na kuubadilisha mfumo uliokuwa umezoeleka kwa wanyeji. Watu hao waliojulikana kama Americo- Liberians waliwapiga marufuku wananchi wasio na ardhi kupiga kura hadi mwaka 1951. Weah ni mtu wa pili mwenye asili ya Liberia kuwahi kuchaguliwa kuwa Rais.

Mwandishi: Angela Mdungu/AFPE

Mhariri: Yusuf Saumu