1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaLibya

Libya yatarajia makubaliano ya sheria mpya za uchaguzi

5 Juni 2023

Viongozi wa Libya wanatarajiwa kukutana nchini Morocco kuhitimisha hatua ya kupata makubaliano kuhusu sheria mpya za Uchaguzi.

https://p.dw.com/p/4SDNM
Libyen | Tripoli
Picha: MAHMUD TURKIA/AFP

Ingawa kutangazwa kwa makubaliano yoyote kuhusu sheria ya kupiga kura au serikali mpya ya mpito huenda kukazusha upinzani unaoweza kusababisha kucheleweshwa zaidi kwa mchakato wa kisiasa.

Tayari wajumbe wa baraza la wawakilishi na baadhi ya wale wa baraza la juu uongozi, hawakubaliani na namna viongozi wao wanavyoendesha majadiliano na wamesema hawatoidhinisha makubaliano yatakayofikiwa. Kwa mujibu wa mwanachama mmoja wa baraza la wawakilishi, Spika wa baraza hilo, Aguila Saleh na mkuu wa baraza la juu la serikali, Khaled al Mishri wamekwenda Morocco na wanatarajiwa kukamilisha mchakato huo wa kupatikana makubaliano.

Soma pia: UN yasema wahamiaji wameteswa na kufanywa watumwa Libya

Viongozi hao wawili wanatarajiwa huenda wakapata makubaliano ambayo kwa namna yoyote yatakuwa yanaumaliza mvutano baada ya miezi kadhaa ya mkwamo. Mjumbe wa Umoja wa Mataifa Adouye Bathily amesema huenda ukafanyika uchaguzi wa kitaifa kufikia mwishoni mwa mwaka huu ikiwa makubaliano yatafikiwa mwezi huu.