Libya yawarudisha wahamiaji wa Misri nchini mwao
1 Februari 2024Msemaji wa chombo hicho Kanali Haytham Belgassem Ammar ameliambia shirika la habari la AFP kwamba mamlaka imeanza mchakato wa kuwarudisha raia 350 wa Misri walioko nchini humo bila vibali.
Mamlaka hiyo ilisema wahamiaji 323 raia wa Nigeriaambao wengi walikuwa wanawake, walirudishwa nchini mwao kutoka mji mkuu Tripoli na mji wa Kaskazini Magharibi Benghazi.
Soma pia:Mpango wa Sunak bado unakabiliwa na changamoto chungunzima
Mwaka jana, tawala hasimu za Libya zilikubaliana kuhusu chombo cha kupambana na uhamiaji kinyume cha sheria.
Libya, taifa linalozongwa na machafuko limekuwa kama kivuko muhimu kwa wahamiaji wanapitia pwani ya Mediterania, kaskazini mwa Afrika, wakitokea sehemu nyingine za Afrika katika safari yao ya hatari wakilenga kufika Ulaya.