1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ligi Kuu England na Italia zaridhia kumaliza msimu

4 Mei 2020

Vilabu vya England juma lililopita vilithibitisha nia ya kuumaliza msimu mara tu vikwazo vya corona vitakapoondolewa. Wachezaji katika ligi hiyo wanaonekana kuwa na hofu kwani bado chanjo ya corona haijapatikana.

https://p.dw.com/p/3blHd
Fußball Champions League | FC Schalke 04 - Manchester City | 2:0 Tor
Picha: Reuters/L. Smith

Huyu hapa Sergio Aguero, mshambuliaji wa klabu ya Manchester City.

"Bila shaka idadi kubwa ya wachezaji wana hofu kwa kuwa wana familia, wana watoto, kwa hiyo natarajia kwamba chanjo itapatikana hivi karibuni ili jambo hili liishe kabisa," alisema Aguero.

Bado kuna mechi 92 hazijachezwa katika ligi hiyo ya England.

Uamuzi kama huo wa vilabu vya England umechukuliwa pia na vilabu vya Italia ambayo iliathirika vibaya na virusi vya corona ila kwa sasa imeanza kuondoa vikwazo vyake polepole kuanzia leo.

Huko Uhispania, wachezaji wataanza kupimwa virusi hivyo kuanzia Jumanne hadi Alhamis na baada ya hapo waanze mazoezi binafsi.