Loew akamia 'kufa na mtu'
12 Novemba 2011- Loew akifanyia majaribio kikosi chake
- Kandanda la Afrika
- London kuwa mwenyeji wa mashindano ya riadha ya dunia 2017
Kikosi cha majaribio cha Ujerumani kililazimika kufanya kazi ya ziada baada ya Ukraine kuongoza kwa Ijumaa usiku ilicheza bila ya wachezaji nyota Bastian Schweinsteiger na Miroslav Klose wenye majereha ya goti na nahodha Philipp Lahm pia akalazimika kupumzika baada ya kushikwa na mafua kutokana na baridi kali.
Barani ulaya zilichezwa pia mechi kadhaa za mwisho za mtoano kusaka tiketi ya fainali za kombe la Ulaya 2012. Croatia iliibwaga Uturuki nyumbani kwao mjini Istanbul mabao 3-0 na Ireland kuitandika Estonia iliocheza mwishowe na wachezaji 9 tu mabao 4-0. Jamhuri ya Cheki iliitandika Montenegro 2-0 Ureno ikatoka sare bila kufungana na Bosnia Herzogovina
Tanzania ilijiwekea matumaini ya kuingia katika orodha ya michuano ya makundi kuwania tiketi ya kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia 2014 nchini Brazil. Timu ya Taifa ya nchi hiyo Taifa Stars iliilaza Chad mabao 2-1 mjini Ndjamena ikihitaji sare tu katika mchezo wa marudiano wiki moja ijayo.
Katika michuano mengine ya mashindano hayo Comoro ikicheza nyumbani ilikandikwa bao moja na Msumbiji,bao la mapema ala mkwaju wa Penalty lililopachikwa na Miro Lobo.. Rwanda ikicheza nyumbani ilitoka sare na Eritrea bao moja kwa moja baada ya Eritrea kuzongoza na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ikaibwaga Swaziland mabao 3-1.
Ama mvua ya magoli iliimiminikia Sao Tome ilipokandikwa na Jamhuri ya Congo mabao 5-0 mjini Brazzaville, huku Namibia ikiipa funzo Djibouti la mabao 4-0. Burundi ilipigwa na mshangao akirudi nyumbani na pigo la bao moja kwa bila mbele ya wenyeji wao Lesotho mjini Maseru.Kenya iliishinda Seychelles 3-0 mabao yaliopachikwa na Pascal Ochieng, Kevin Kimani na Dennis Oliech .
Mchezaji wa kimataifa Emmanuel Adebayor amekua akijadiliana na maafisa wa chama cha soka cha Togo juu ya uwezekano wa kurudi tena katika timu ya taifa. Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la utangazaji la Uingereza BBC, mshambuliaji huyo ambaye anaichezea Tottenham Hotspur ya Uingereza kwa mkopo kutoka kilabu ya Mancheaster City alistaafu timu ya taifa baada ya basi la timu hiyo ya Togo kushambuliwa siku chache kabla ya kuanza fainali za kombe la mataifa ya Afrika nchini Angola. Watu wawili katika kikosi cha timu hiyo waliuawa na Togo ikajitoa mashindanoni.
Togo iliocheza fainali za kombe la dunia 2006 imeshindwa kufuzu kucheza fainali za mwaka ujao za kombe la mataifa ya Afrika-mashindano yatakayoandaliwa kwa ubia nchini Gabon na Guinea ya Ikweta. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amewahi pia kucheza Arsenal na Real Madrid. Pindi akikubaliana na maafisa wa chama cha kandanda cha Togo, ataweza kucheza mechi muhimu ya marudiano dhidi ya Guinea Bissau, ya kuwania nafasi ya kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia 2014, Jumanne ijayo mjini Lome.
Ivory Coast au Cote d´Ivoire ambayo iko nafasi ya juu katika orodha ya timu zenye kiwango kikubwa cha mchezo barani Afrika katika dimba, leo inawania kumaliza mwaka kwa mafanikio, wakati itakapochuana na Afrika kusini katika mchezo wa kirafiki mjini Port Elizabeth .Timu ya taifa ya Ivory Caoast Tembo iliojaa wachezaji maarufu katika ligi kuu ya England imezishinda Benin mara mbili, Rwanda na Burundi katika kujinyakulia nafasi ya mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka ujao na kuzibwaga pia Mali na Israel katika mechi za kirafiki.
Miongoni mwa majina maarufu ni ndugu awawili Kolo na Yaya Toure wanaocheza Manchester City, Gervinho Arsenal na Salomon Kalou anayelisakata gozi katika kilabu ya Chelsea. Afrika kusini imeshinda mara moja na kwenda sare mechi tatu katika kombe la mataifa ya Afrika na za kirafiki dhidi ya Cote d`ivoire, tangu 1994 zilipotoka sare bila kwa bila mjini Port Elizabeth.
Afrika Kusini imeshatolewa katika fainali za kombe la mataiafa ya Afrika, mashindano yatakayoandaliwa kwa ubia na Gabon na Guinea ya Ikweta mwakani, baada ya matokeo ya sare ya kutofungana na Sierra Leone kuifungisha virago na kuipa nafasi Niger.
Mechi ya leo dhidi ya Cote d´Ivoire itashuhudia kurudi uwanjani kwa nahodha wa Bafana Bafana na mchezaji wa kiungo wa Tottenham Hotspur Steven Pienaar, ambaye alilikosa pambano dhidi ya Niger na pia na Sierra Leone kwa sababu ya majeraha.
Kocha wa zamani katika ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga, Christoph Daum amekubali kusaini mkatabana kilabu ya Ubeligi ya Bruges, kukiwa na mwanya unaompa nafasi ya kuongeza kwa mwaka mmoja, pale utakapomalizika Juni mwaka ujao. Daum mwenye umri wa miaka 58 ni kocha wa zamani wa Bayer Leverkusen, FC Cologne, na VFB Stuttgart ambapo ilishinda taji la ubingwa 1992.
Hadi karibuni alikuwa kocha wa Eintracht Frankfurt, lakini akaondoka baada ya kushuka daraja la pili msimu huu. Daum pia amefundisha soka Uturuki akishinda mataji ya ubingwa pamoja na Fenerbahce na Besiktas. Alikua Kocha pia nchini Austria ambapo Austria Vienna ilishinda ubingwa. Katika kilabu ya Bruges alikoanza kazi juma hili, amechukua nafasi ya Mholanzi Adrie Koster . Bruges ni mabingwa mara 13 wa ligi kuu ya Ubeligiji. Lakini safari hii imecheza mechi 6 za ligi bila ya ushindi licha ya kuongoza kundi lake katika ligi ya Ulaya.
Riadha:
Jiji la London liatakua mwenyeji wa mashindano ya riadha ya Ubingwa wa dunia 2017. Mji mkuu huo wa Uingereza ulishinda kinyangayiro hicho dhidi ya mji mkuu wa Qatar Doha kwa kura 16 dhidi ya 10 iliofanyika mjini Monaco. Itakumbukwa London pia ni mwenyeji wa michezo ijyo ya Olimpik 2012.
Wakati huo huo mji wamwambao wa kaskazini mwa Poland SOPOT ndiyo utakaoandaa mashindano ndani ya riadha 2014. Shirikisho la kimataifa la mchezo wa riadha IAAF pia limeupa nafasi mji wa Marrakech nchini Morocco kuwa mwenyeji wa mashindano ya kombe la Shirikisho 2014. nayo mashindano ya dunia ya ubingwa wa riadha kwa vijana yatafanyika mjini Oregon-Marekani 2014.
Ubondia:
Ulimwengu wa michezo wiki hii uliomboleza kifo cha bingwa wa zamani wa ndondi uzani wa juu Joe Frazier aliyefariki dunia usiku wa Jumatatu kutokana na saratani ya figo. Fzaizier atakumbukwa kwa pambano lake kabambe ana la kihistoria dhidi ya mfalme wa ndondi Muahammad Ali .
Mwezi Machi mwaka 1971 walizipiga katika ukumbi wa Madison Square ambapo mabondia wote wawili walilazwa hospitali baada ya pambano hilo. Fraizier alilimudu pambano hilo na kumshinda Ali kwa pointi akiushangaza ulimwengu, akipa dunia moja wapo ya misisimko mikubwa isiyowahi kushuhudiwa katika mchezo huo wa ndondi.
Frazier hata hivyo alishindwa na Ali katika pambano la marudiano katika ukumbi huo, kabla ya kuandaliwa pambano jengine la kusisimua 1975 mjini Manilla. Mmoja kati ya watu waliotoa rambirambi zao ni Ali aliyesema "Dunia imempoteza bingwa muhimu. Nitamkumbuka Joe kwa heshima na taadhima. rambirambi zangu nyingi nazituma kwa familia na wanaompenda,"
Joe Fraizier amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 67.