1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Waziri mkuu wa Uingereza anataka sheria ngumu zaidi kwa watu wanaochochea ugaidi.

13 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEun

Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair amesema kuwa serikali yake itaangalia mara moja uwezekano wa kuchukuliwa hatua kali zaidi dhidi ya watu wanaochochea ama kushawishi watu kufanya ugaidi.

Akizungumza katika bunge baada ya shambulio la wiki iliyopita la mabomu dhidi ya mji wa London, Blair amesema hatua hizo ni pamoja na utaratibu mgumu zaidi wa watu kuingia nchini humo.

Ameongeza kuwa ushirikiano mkubwa zaidi dhidi ya ugaidi unahitajika kati ya mataifa ya umoja wa Ulaya.

Wakati huo huo , waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza Charles Clarke yuko mjini Brussels ambako atakuwa mwenyekiti wa mkutano maalum wa mawaziri wa mambo ya ndani wa umoja wa Ulaya utakaojadili kile kinachoonekana kuwa ni tukio la shambulio la kwanza la kujitoa muhanga katika Ulaya ya magharibi.

Jana , polisi wamesema kuwa wamewatambua watuhumiwa wanne, wanaoaminika kuwa ni raia wa Uingereza wenye asili ya Pakistan. Mmoja kati yao amekamatwa katika msako mkubwa unaoendelea ndani na nje ya mji wa Leeds.