1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Waziri mkuu wa Uingereza, Tony Blair, ashindwa bungeni

10 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEJu

Waziri mkuu wa Uingereza bwana Tony Blair, ameshindwa kwa mara ya kwanza bungeni juu ya mpango wake wa kuziongezea nguvu sheria dhidi ya ugaidi. Wabunge 322 waliyaunga mkono mapendekezo yake ya kuwazuilia washukiwa wa ugaidi kwa siku 90 bila kushtakiwa, huku wengine 291 wakiyapinga.

Wabunge takriban 40 wa chama chake Blair cha Labour, waliyapinga mapendekezo hayo. Wadadisi wanasema matokeo ya kura hiyo yameathiri mamlaka aliyonayo waziri Blair. Lakini Blair, ambaye anakutana hivi sasa na wakuu wa polisi na ukachero, amepinga madai hayo.

Wakati huo huo, wabunge waliiidhinisha kurefushwa kwa mda wa kuzuiliwa mshukiwa kutoka siku 14 hadi 28. Polisi wa Uingereza waliitisha mamlaka mapya baada ya wanamgambo wa kiismalu wa kujitoa muhanga kuwaua watu 52 mjini London mnamo tarehe 7 mwezi Julai. Wakosoaji wanasema mamlaka hayo mapya yataathiri uhuru wa raia katika jamii.