1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Waziri Mkuu wa Uingereza, Tony Blair, atang'atuka mwezi ujao.

10 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC3R

Waziri Mkuu wa Uingereza, Tony Blair atang’atuka wadhifa wake tarehe 27 mwezi Juni.

Tony Blair alitangaza hayo katika eneo lake la uwakilishi bungeni la Sedgefield kaskazini mwa Uingereza.

Tony Blair amesema:

"Nimewasili hapa Segdefield katika eneo langu la bunge ambako nilianzia harakati zangu za kisiasa na ambako bila shaka ninapaswa kuzimalizia.

Leo hii ninatangaza kwamba nitang’atuka kutoka uongozi wa chama cha Leba. Chama sasa kitamchagua kiongozi mpya. Tarehe ishirini na saba mwezi Juni nitampelekea Malkia barua ya kujiuzulu wadhifa wa Waziri Mkuu"

Hapo awali Tony Blair alikuwa amelihutubia baraza lake la mawaziri kuhusu uamuzi wake huo.

Waziri Mkuu huyo aliwataka radhi wafuasi wake kwa uamuzi ambao amekuwa akichukua akiuzingatia kuwa muhimu lakini ambao umekuwa ukizusha kutoelewana nchini mwake.

Waziri wa fedha, Gordon Brown, anatarajiwa kuchukua wadhifa wa kiongozi wa chama cha Leba na pia uwaziri mkuu pale Tony Blair atakapoondoka madarakani.