LONDON: Waziri mkuu wa Uingereza,Tony Blair, apinga uchunguzi wa sasa hivi juu ya kushiriki kwake katika vita vya Irak
1 Novemba 2006Matangazo
Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair amesema hapingi kufanyike uchunguzi juu ya vita vya uvamizi nchini Irak mwaka wa 2003. Lakini akizungumza mbele ya baraza la wawakilishi, Blair amesema kufanya hivyo sasa hivi, itakuwa ishara mbaya kwa washirika wa Uingereza katika vita hivyo vya Irak. Tamko hilo limetolewa masaa machache baada ya serikali yake kupata ushindi katika kura bungeni ya kutaka kufanyike uchunguzi juu ya sera za serikali ya Uingereza kuhusu Irak. Mswada wa sheria juu ya hilo, ulikuwa umewasilishwa bungeni na chama cha upinzani cha konsevative na vyama vya kihafidhina vya Scotland na Wales.