1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Tume ya haki za binadamu yataka Myanmar iwekewe vikwazo

1 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/CBL3

Tume ya kimataifa kutetea haki za binadamu Amnesty International imelitaka baraza la usalama la umoja wa mataifa kuchukuwa hatua za kuweka vikwazo vya silaha dhidi ya serikali ya kijeshi ya Myanma.

Tume hiyo pia imezitaka China na India ikiwa ndizo nchi zinazouza silaha kwa kiwango kikubwa nchini Myanmar kusitisha zoezi hilo hadi pale utawala wa kijeshi utakapo rekebisha haki za kibinadamu.

Wiki iliyopita vikosi vinavyotii utawala wa kijeshi vilitumia risasi dhidi ya waandamanaji wanaounga mkono harakati za kidemokrasia zinazopinga utawala huo wa kijeshi.

Mamia ya waandamanaji pamoja na watawa wa madhehebu ya Budha wamekamatwa na kuwekwa kizuizini.

Mjumbe maalum wa umoja wa mataifa bwana Ibrahim Gambari anatarajiwa at kesho kukutana na mkuu wa kijeshi nchini Myanmar jenerali Than Shwe.

Bwana Gambari amesisitiza umuhimu wa mazungumzo baina ya utawala wa kijeshi na wapinzani.