1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LOS ANGELES:Mamake mshtaki wa Michael Jackson akabiliwa na mashataka ya udanganyifu

24 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEiM

Mamake kijana aliyemshtaki mwanamuziki nyota wa Marekani Michael Jackson kwa madai ya kumlawiti ameshtakiwa kwa udaganyifu na mahakama moja nchini humo.

Kiongozi wa mashataka amesema kwamba mama huyo alidanganya juu ya hali yake ya kifedha alipoandika maombi ya kutaka msaada wa kifedha kutoka kwa serikali.

Mama huyo ambaye jina lake limefichwa na mashirika mengi ya habari ya Marekani alikataa kutoa ushahidi juu ya hali yake ya kifedha kwenye kesi iliyomhusu Michael Jackson lakini mtetezi wa Michael Jackson alishikilia kwamba mwanamke huyo ni laghai na ana mtumia mwanawe ili kudanganya juu ya kesi dhidi ya Jackson ili ajipatie pesa jambo ambalo sasa anasema limejitokeza wazi.

Mwanamke huyo inadaiwa alijipatia dola elfu 18 baada ya kutuma maombi ya uwongo kwa huduma ya serikali ya kutaka usaidizi kutokana na hali yake duni ya kifedha.

Iwapo atapatikana na hatia atakabiliwa na kifungo cha miaka mitano jela.