1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lukashenko atangaza kugombea urais mwaka 2025

Sylvia Mwehozi
25 Februari 2024

Kiongozi wa Belarus, Alexander Lukashenko amesema atagombea tena uchaguzi mwaka 2025. Tangazo hilo limetolewa mapema siku ya Jumamosi na shirika la habari la Belarus BeITA.

https://p.dw.com/p/4cr6a
Lukaschenko akiwa mjini Minsk
Rais wa Belarus, Alexander Lukashenko Picha: Alexander Zemlianichenko/AP/picture alliance

Kiongozi wa Belarus, Alexander Lukashenko amesema atagombea tena uchaguzi mwaka 2025. Tangazo hilo limetolewa mapema siku ya Jumamosi na shirika la habari la Belarus BeITA. Lukashenko ametoa tamko hilo mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kushiriki kupiga kura za bunge na serikali za mitaa.

Soma: Lukashenko adokeza kupelekwa silaha za nyuklia kutoka Urusi

Akiendelea kujibu maswali ya waadishi wa habari amesema kuwa atatetea kiti chake kwa kuwa hakuna mtu, wala rais mwajibikaji anayeweza kuwaacha raia wake waliomuunga mkono wakati wa mapambano.

Rais huyo mwenye miaka 69 ameitawala Belarus tangu mwaka 1994 na ni mmoja wa washirika wa karibu wa Rais wa Urusi Vladimir Putin. Hata hivyo aliongeza kuwa mwaka mmoja hadi kufanyika kwa uchaguzi wa rais ni kipindi kirefu na mambo mengi yanaweza kubadilika.