SiasaBrazil
Lula kuzungumza na Biden kuhusu uchaguzi wa Venezuela
30 Julai 2024Matangazo
Kwa mujibu wa ikulu ya Marekani na serikali ya Brazil, mazungumzo hayo yalitarajiwa kufanyika mwendo wa saa nane na nusu saa za Marekani, lakini mada zitakazojadiliwa hasa, hazikutajwa. Kwa mujibu wa duru nchini Brazil, mazungumzo hayo ya simu yalipwangwa kufuatia ombi la serikali ya Marekani, huku ikijaribu kutafuta tathmini ya Brazilkuhusu matokeo ya uchaguzi katika taifa jirani yake la Venezuela. Utawala wa Kremlin kupitia Dmitry Peskov, mkuu wa kitengo cha habari cha rais Vladimir Putin, leo umeutaka upinzani Venezuela ukubali matokeo. Mamlaka ya uchaguzi Venezuela ilimtangaza rais Nicolas Maduro mshindi kwa asilimia 51.2 ya kura.