Lusaka. Makamu wa rais wa zamani asimamishwa uanachama katika chama tawala nchini Zambia.
9 Aprili 2005Matangazo
Chama tawala nchini Zambia kimemsimamisha uanachama makamu wa zamani wa rais kwa kumshutumu rais Levy Mwanawasa kuwa ni mla rushwa, katika juhudi zinazoonekana ni za kuinua hadhi ya kiongozi huyo dhidi ya mpinzani anayeonekana kuwa muhimu.
Chama cha Movement for Multiparty Democracy MMD, kimemsimamisha Nevers Mumba ambaye madai yake ya rushwa yanakuja wakati kunafanyika uchaguzi wa ndani hapo May katika chama hicho ambapo anapambana na rais wa sasa Levy Mwanawasa katika wadhifa wa kiongozi wa chama. Uchaguzi mkuu wa rais na bunge unatarajiwa kufanyika mwakani.