1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lusaka. Uhaba wa petroli waikumba Zambia.

2 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEVg

Serikali ya Zambia imesema leo kuwa inajaribu kutatua matatizo ya uhaba wa mafuta ya petroli ambao umesababisha mkwamo katika usafiri wa umma na vituo vya kuuzia mafuta vikiwa havina bidhaa hiyo.

Upatikanaji wa petroli nchini Zambia umeshuka sana katika muda wa siku nne zilizopita baada ya kinu pekee nchini humo cha kusafishia mafuta mjini Ndola , kiasi cha kilometa 400 kaskazini ya mji mkuu Lusaka , kukumbwa na matatizo wakati wa ukarabati na kusababisha kufungwa kwa muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa.

Waziri wa nishati George Mpombo ameliambia shirika la habari la AFP kuwa serikali inafanya kila linalowezekana kuweza kutatua tatizo hilo.

Bwana Mpombo amesema kuwa makampuni ya kuuza mafuta yameruhusiwa kuagiza moja kwa moja mafuta yaliyosafishwa nchini humo ili kuweza kuondoa tatizo hilo.

Watu wenye magari wameendelea kubaki katika milolongo ya kungojea mafuta katika vituo vya kuuzia mafuta na wengine hulala katika magari yao wakisubiri mafuta. Wamiliki wa mabasi ya abiria wamelazimika kusitisha huduma hiyo.