Hali ya wasiwasi imetanda katika miji midogo ya Kalengera na Rubare huko wilayani Rutshuru mkoani Kivu kaskazini katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo ambako mapigano makali yanaendelea kati ya jeshi la Congo na waasi wa M23. Kutaka kupata picha kamili kuhusu jinsi hali ilivyo kufikia sasa, Tatu Karema amezungumza na mwandishi wa DW kutoka Goma, Benjamin Kasembe.