MAAFIKIANO YA KUGAWANA MALI
24 Desemba 2003Matangazo
NAIVASHA: Serikali ya Sudan na waasi wa kusini SPLA,kimsingi wamekubaliana vipi watagawana utajiri wa nchi hiyo,vita vya wenyewe kwa wenyewe vitakapomalizika.Hayo amearifu waziri wa kigeni wa Kenya Kalonzo Musyoka.Hiyo ni ishara kuwa kumepatikana maendeleo makubwa katika mazungumzo ya amani mjini Naivasha.Mkataba wa amani utaondosha kikwazo kikubwa cha kukomesha vita hivyo vya miaka ishirini katika nchi kubwa kabisa barani Afrika.Watu milioni 2 wamepoteza maisha yao na milioni 4 wengine wamelazimika kuondoka makwao kwa sababu ya vita hivyo.