MigogoroMashariki ya Kati
Watu 19 wameuawa kwenye mashambulizi ya Israel huko Gaza
4 Januari 2025Matangazo
Shirika la Ulinzi wa Raia limesema shambulizi la anga mapema Jumamosi, liliilenga nyumba ya familia ya al-Ghoul katika Mji wa Gaza na kuwauwa watu 11, saba kati yao wakiwa ni watoto. Msemaji wa shirika hilo Mahmud Bassal amesema nyumba hiyo ya ghorofa mbili, iliyokuwa imewahifadhi watu kadhaa waliopoteza makazi yao, iliharibiwa kabisa.
Jeshi la Israel halijazungumzia mashambulizi hayo. Kwingineko, shirika la ulinzi wa raia limesema maafisa watano wa usalama, waliopewa jukumu la kuongozana na misafara ya msaada, waliuawa kwenye shambulizi la Israel wakati wakisafiri kwenye gari katika mji wa kusini wa Khan Yunis. Jeshi la Israel halijajibu tuhuma hizo.